Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo Hamis Mwinjuma amesema kamati ya kutafuta vazi la Taifa tayari imekamilisha kazi yake, na imerudisha mrejesho wizarani kupitia Idara ya Maendeleo na Utamaduni ambayo nayo imefikia hatua za mwisho za kukamilisha mchakato huo ili kulitangaza vazi la Taifa.
Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri Mwinjuma amesema ni hamu ya wengi kuona mchakato huo umekamilika.
Amelihakikishia Bunge kuwa hatua zilizofikiwa hivi sasa ni za mwishoni na kwamba kabla ya mwaka huu kuisha vazi hilo litakuwa limetangazwa.
Kutazama video bofya kiunganishi (link) hapo chini
https://www.instagram.com/reel/C3C09d8OnCT/?igsh=cGJudGE3cWt6YW