Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kutokana na utafiti alioufanya amezitaja kazi kuu sita duniani ambazo zinahitajika zaidi.
Kazi hizo ni Software developer, Data scientist, Information Security Analyst, Nurses, Management Analyst na Artificial Intelligence Specialist.
Amesema kazi hizo zote zinategemea uchumi na ndio sababu nchi zenye uchumi mkubwa ndio zinaweza kufanya vizuri katika maeneo hayo na kuongeza kuwa kama nchi itahitaji kuwa na uchumi shindani ni lazima isomeshe watu na iheshimu tafiti na wasomi.
Profesa Muhongo ameitaja India kama nchi ya mfano ambayo amesema imeshika nafasi ya tano kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani kwa sababu vijana wake wameweka kipaumbele katika masomo ya Data scientist, Blockchain engineering, Digital Marketing, Machine Engineering na Artificial Inteligence.
Kutazama video yake bofya (link) kiunganishi hapo chini
https://www.instagram.com/reel/C3CysfEOEim/?igsh=aW52ampzbmFreW91