Nani kuwa bingwa wa AFCON 2023

0
301

Zilikuwa siku 12 za moto katika soka la Afrika ambapo mataifa 24 yalishuka dimbani mara 36, kila moja likicheza mechi tatu, kutafuta nafasi ya kuwania kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2023).

Tayari timu 16 zilizofuzu zimepatikana, timu nane zimeaga mashindano, na hatua inayofuata ni kutafuta timu nane zitakazofuzu robo fainali na kuendelea hadi kumpata bingwa.

Baada ya kukiona Kipute Mserereko kwenye hatua ya makundi, je, karata yako ya ubingwa unaiweka kwa nani? Au bingwa wako uliyemtabiri ametolewa?

Mechi zote 52 zinakujia kupitia TBC1, TBC2, Tanzania Safari Channel, TBC Taifa na TBC FM.

AFCON2023 #KiputeMserereko #TBCupdates #TBCdigital