Rais John Magufuli ameanza ziara ya kikazi ya siku Nane mkoani Mbeya, baada ya kurejea nchini kutoka nchini Malawi ambapo alikua na ziara ya kikazi ya siku Mbili.
Baada ya kuwasili mkoani Mbeya, Rais Magufuli akiwa na mke wake Mama Janneth Magufuli amepokelewa na Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila.
Akiwa mkoani humo, Rais Magufuli amewapongeza wakazi wa mkoa wa Mbeya kwa kufanya kazi kwa bidii na pia ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya mkoa huo.
Rais Magufuli amewaahidi Wakazi wa mkoa wa Mbeya waliojitokeza kumpokea kuwa, serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.