Lindi yaahirisha maadhimisho ya siku ya Malaria

0
474

Kufuati tishio la Kimbunga Kenneth katika mikoa ya  Mtwara na Lindi, mkoa wa Lindi umetangaza kuahirishwa kwa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyokua yafanyike mkoani humo.

Akitangaza Uamuzi huo, Mkuu wa mkoa wa Lindi, –  Godfrey Zambi amesitisha pia shughuli zote za serikali na kuwataka wakazi wa mkoa  huo kuacha kupuuza tahadhari inayoendelea kutolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuhusu kimbunga Kenneth.