Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemulekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof.Jamali Katundu amsimamishe kazi Afisa Manunuzi wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Lindi, Kennedy Mbagwa, kwa kushindwa kusimamia mitambo ya uchimbaji visima na ununuzi wa pikipiki ambazo zimeachwa katika stoo za RUWASA mkoani humo tangu mwaka 2021.
Kutotumika kwa vitendea kazi hivyo kumebainika wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ofisi za RUWASA mkoani Lindi.
Pamoja na hilo, amesema tathmini itafanyika katika mamlaka zote za maji kujua zinadaiwa kiasi gani na zinadai kiasi gani ili makusanyo yanayofanyika yalete matokeo ya kazi kwa wananchi.
Aweso amewataka watendaji katika sekta ya maji kila mmoja atimize wajibu wake katika kuwahudumia wananchi.