SGR Tanzania hadi Burundi ipo hatua za manunuzi

0
403

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema mradi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza-Msongati – Gitega (Burundi) umefikia hatua ya manunuzi.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa katika mkutano wa wakandarasi na waziri wa nchi, ardhi, miundombinu, uchukuzi na utalii kutoka Japan.

Mabrawa amesema hivi sasa Tanzania inaendela na ujenzi wa SGR ambapo ujenzi wake kwa awamu ya kwanza umeanza kipande kinachoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza (kilomita 1,219) huku awamu ya pili kipande cha Tabora – Kigoma (kilomita 506) kikiwa katika hatua za maandalizi na awamu ya tatu Uvinza – Msongati – Gitega (kilomita 282) na Isaka -Rusumo-Kigali (kilomita 495) vikiwa katika hatua za manunuzi.

Sambamba na hilo ameongeza kuwa Tanzania inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi yake ya kimkakati ya SGR kutoka Isaka – Rusumo – Kigali (kilomita 495) na Kaliua – Mpanda – Karema (kilomita 317), pamoja na miradi mingine ya reli kutoka Mtwara – Songea – Mbambabay (kilomita 1,000) na Tanga – Arusha – Musoma (kilomita 1,028).