Ekari 100 zatengwa kwa waathirika wa Hanang

0
364

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda ametembelea na kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia waathirika wa maporomoko ya tope wilayani Hanang, mkoani Manyara.

Jumla ya ekari 100 kutoka Jeshi la Magereza kwenye eneo la Warret zimetolewa kwa ajili ya waathirika hao ambapo viwanja 269 vimepimwa na kupandwa mawe.

Serikali inatarajiwa kujenga nyumba 101 kwa ajili ya waathirika ambapo kila moja itakuwa na vyumba vitatu.