TBC kukuletea mbashara uzinduzi wa Ruangwa FM

0
339

Timu ya watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ipo wilayani Ruangwa mkoani Lindi kwa ajili ya kukuletea mbashara uzinduzi wa kituo cha redio, Ruangwa FM, Januari 6, 2024.

Kituo hicho cha redio kimeboreshwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa.

Usikae mbali ya kurasa za mitandao ya kijamii ya TBC Digital kufahamu mengi zaidi juu ya tukio hilo muhimu kwa kijamii.