SERIKALI KUJENGA KITUO CHA AFYA HANANG

0
367

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa na timu kutoka wizara ya afya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga wametembelea eneo lililoathirika na maporomoko ya matope yaliyopelekea vifo vya watu 89 na majeruhi 139 wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Katika ziara hiyo amebainisha mambo kadhaa yatakayoendelea kutekelezwa na Serikali ikiwemo kupeleka magari matatu ya kubebea wagonjwa na kujenga kituo cha afya katika eneo lililotengwa na Serikali kwa makazi ya watu.

“Serikali itaendelea kuwahudumia majeruhi waliobakia kwa sasa ambao ni watano kwa gharama za Serikali kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Waziri Ummy.