RAIS AANZISHA MPANGO WA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI

0
276

Rais Samia Suluhu Hassan ameanzisha mpango wa madaktari bingwa kwenda kuwajengea uwezo watumishi katika vituo vya afya ili waongeze utendaji wao katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo mkoani Tanga na kufafanua kuwa “mpango huu ni mahususi kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuimarisha utoaji wa huduma bora katika vituo vya afya kote nchini.”

Amesema ili kufanikisha mpango huo, shilingi bilioni 625 kutoka Benki ya Dunia zitatumika kuhakikisha mpango huo unakuwa endelevu na kuvifikia vituo ambavyo havijafikiwa nchi nzima.

“Hii ni awamu ya pili ya Madakitari Bingwa wa Mama Samia wanaozunguka katika vituo vya Afya kote nchini kwa kutoa huduma na kuwajengea uwezo watumishi ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao,” amesema.