ANDAENI ANDIKO KUSHAURI USIMAMIZI WA MAJUKUMU

0
475

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuandaa mwongozo wa usimamizi wa majukumu ya maafisa wake.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo alipokuwa akihutubia maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii na kilele cha Wiki ya Ustawi wa Jamii Mkoani Dar es Salaam.

Amesema maafisa hao wanapoajiriwa hufanya kazi chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa aliyepo Wizara ya Afya jambo ambalo halileti muunganiko wa usimamizi wa majukumu ya maafisa ustawi wa jamii.

Aidha ameitaka wizara hiyo kuandaa andiko litakalomashauri Rais Samia Suluhu Hassan vile inavyopaswa kwa kuwa lengo la kuundwa kwa wizara hiyo ni kusimama yenyewe ili iweze kutekeleza majukumu yake.