TAARIFA KWA UMMA

0
325

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya llemela imeona taarifa ya picha ikisambaa katika mitandao ya kijamii kionyesha kuwa katika kituo cha Afya cha Buzuruga wakinamama wamekuwa wakipeana zamu kuzalia sakafuni‚ aidha taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikifafanua kuwa picha iliyotumika katika taarifa hiyo ni ya
Septemba 2022.

Awali katika Kituo hiki cha Afya cha Buzuruga kulikuwa na vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia, baada ya kuona kumekuwa na ongezeko la wakinamama wanaojifungua Serikali iliongeza idadi ya vitanda vya kujifungulia kutoka vitanda vitatu hadi vitanda sita.

Sambamba na hilo Serikali imejenga jengo la mama na moto lenye uwezo wa kulaza wakinamama 42, jengo hilo liligharimu kiasi cha shilingi Milioni 200 fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

Lengo ikiwa ni kuondoa adha ya wakinamama kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja na jengo hilo lilizinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ambalo kwa sasa linatumika.
Hivyo kwa maelezo hayo,Halmashauri ya Manispaa ya llemela, inapenda kuuhakikishia umma kuwa katika kituo cha Afya cha Buzuruga, hakuna wakina mama wanaojifungulia chini kama taarifa ya mtandaoni inavyoonyesha.