Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeahidi kuchangia shilingi milioni 97 katika Taasisi ya Profesa Jay yenye lengo la kuisaidia jamii katika matibabu ya ugonjwa wa figo.
Hayo hamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel katika uzinduzi wa taasisi hiyo akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akifafanua mchango huo wa Serikali Dkt. Mollel amesema shilingi milioni 50 zitakwenda moja kwa moja kwenye taasisi na shilingi milioni 47 ni kwa ajili ya matibabu ya Prof. Jay ikiwa atahitaji kupandikiza figo.
Katika uzinduzi huo Dkt. Mollel aliwasilisha ahadi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika taasisi ya Profesa Jay ya kuchangia shilingi milioni 10.