Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewajulia hali majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Tumaini wilayani Hanang kwa kuwapa pole pamoja na kuwatakia afya njema.
Rais Dkt. Samia ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel pamoja na viongozi na watendaji wengine.
Aidha, amewapongeza wataalam wa afya kwa kuwahudumia vyema majeruhi pamoja na wagonjwa wanaofika hospitalini kwa ajili ya kupata matibabu.