Idadi ya waliofariki katika mafuriko yaliyotokea Katesh, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara imeongezeka kufikia 76 ambapo jumla ya majeruhi ni 117, huku baadhi wakiwa wameruhusiwa kutoka hospitali na kaya zilizoathiriwa ni 1,150.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Katesh, baada ya Rais Samia kutembelea waathirika na majeruhi wilayani humo.
Pia, Waziri Jenista amesema walioathiriwa wote wanapatiwa matibabu bure na gharama za matibabu zinabebwa na Serikali.