Mashabiki wa Arsenal wameanzisha kampeni inayolenga kukusanya Pauni milioni 25 (TZS bilioni 78) kwa ajili ya kuiongezea Wes Ham United, kwa madai kuwa fedha ambayo Arsenal ililipa, Pauni milioni 105 (TZS bilioni 330) kumsajili Declan Rice haiendani na thamani ya kiwango ambacho nyota huyo anaonesha.
Raia huyo wa Uingereza amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Arsenal alichojiunga nacho majira ya joto, ambapo moja ya mchango wake ni gli la dakika ya 90+7 lililoiwezesha Arsenal kuondoka na ushindi wa 4-3 dhidi ya Luton Town.
Mashabiki wanaona kama Arsenal imewazulumu West Ham kwa kumpata Rice kwa bei rahisi.