MGOGORO WA ARDHI KIEGEYA WAMALIZWA

0
241

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imemaliza na kuufunga mgogoro wa ardhi wa wananchi 767 wa Kiegeya mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda amemaliza na kuufunga mgogoro huo alipokutana na wawakilishi wa wakulima wakiongozwa na Mwenyekiti wao Haleluya Minga katika ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro.

Pinda amefika mkoani humo kwa ajili ya kuwasikiliza ili kupata ukweli na kubaini udanganyifu katika maelezo ya wakulima na kuwapa taarifa kuwa mwekezaji ni mmiliki halali na alitoa ekari 4000 alizoombwa na serikali na wao wamevamia sehemu mpya.

Wananchi hao walivamia na kulima katika shamba la Tungi Sisal Estate la Mwekezaji Star Infrastructure.