Uhakika wa matibabu majeruhi wa maafa Hanang 100%

0
251

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amewahakikishia majeruhi wa maafa ya maafuriko wanaotibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini pamoja na vituo vingine vya kutolea huduma wilayani Hanang kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba upo kwa asilimia 100 na hakuna mgonjwa yeyote atatozwa fedha kwa ajili ya matibabu.

Dkt. Dugange ameyasema hayo alipotembelea hospitali hiyo kuangalia hali za majeruhi sambamba na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Katika hatua nyingine, Dkt. Dugange alikuwa miongoni mwa viongozi walioambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwajulia hali manusura wa maafa ya mafuriko waliotengewa eneo katika Shule ya Sekondari Katesh.