Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mafuriko yaliyotoke wilayani Hanang mkoa wa Manyara imeongezeka na kufikia watu 49 baada ya kupatikana kwa miili mingine miwili.
Taarifa ya Mkuu wa mkoa Manyara, Queen Sendiga aliyotoa asubuhi hii Desemba 4, 2023 imesema idadi ya majeruhi bado ni 85.
Ameongeza kuwa shule za msingi za Katesh, Hanang na Dumanang zitatumika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo, na amewataka Wananchi kuhama mara moja maeneo ya hatari ili kujikinga na madhara mengine yanayoweza kutokea.