Msukuma : Geita hatuna matatizo na Rais Samia

0
148

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku (Msukuma) amesema Geita hawana matatizo yoyote na Rais Samia Suluhu Hassan kwasababu yote waliyoyaomba yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi jimboni kwake.

Msukuma ameyasema hayo wakati wa ufungaji wa maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Amesema katika jimbo lake la Geita Vijijini, barabara zimejengwa mpaka mtaani, umeme upo na pia kuna taa zimefungwa katika barabara za jimbo hilo.

Aidha, Msukuma ameomba maonesho hayo ya madini yaendelee kufanyika Geita na kutopelekwa sehemu nyingine kama ilivyo kwa maonesho mengine kama Sabasaba na Nanenane ambayo huzunguka mikoa mbalimbali. Msukuma amesema asili ya Dhahabu ni Geita na mkoa huo unaongoza kwa uchimbaji wa madini hivyo haina haja kuyapeleka maonesho hayo sehemu nyingine