Maafisa wa serikali ya Ivory Coast wameteketeza Tani Elfu 18 za mchele ambao umeonekana haufai kwa matumizi ya binadamu.
Mchele huo uliingizwa nchini Ivory Coast ukitokea Myanmar na kabla ya kuingia nchini humo, meli iliyobeba mchele huo ilikataliwa kutia nanga katika bandari kadhaa za nchi za Afrika Magharibi.
Bandari hizo zipo katika nchi za Togo, Guinea na Ghana.
Baada ya meli hiyo kutia nanga nchini Ivory Coast mchele huo ulishushwa na kupimwa na kubainika kuwa haufai.