Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Mtwara

0
187

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara kuanzia Septemba 14 hadi 17 mwaka huu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas, amesema katika ziara hiyo, Rais Samia atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Aidha, Rais Samia atafuatilia utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wakuu wa serikali pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kuwa yanatekelezwa.

Kufuatia ziara hiyo, Kanali Abbas, amewaomba wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais mara atakapowasili katika mkoa huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara tangu alipoapishwa kuwa Rais Machi 2021.