Balozi Stephen Mbundi ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Balozi Mbundi anachukua nafasi ya Balozi Kennedy Gastorn ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Rais Samia.Suluhu Hassan pia amemteua Balozi Said Shaib Mussa ambaye ni Balozi wa Tanzania huko Kuwait kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Mussa anachukua nafasi ya Balozi Fatma Rajab ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, Oman.
Balozi Kennedy Gastorn yeye ameteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Balozi Gastorn anachukua nafasi ya Dkt. Evaristo Longopa ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano.ya Rais, Ikulu, uteuzi huo umeanza Septemba 03, 2023.