GUNIA SIO KIPIMO “Ni kifungashio”

0
143

GUNIA SIO KIPIMO “Ni kifungashio”

Serikali imesema haitambui gunia kuwa kipimo bali ni kifungashio, hivyo wadau wote ni muhimu wakaepuka kutumia gunia kama kipimo.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exhaud Kigahe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Husna Sekiboko aliyetaka kufahamu kama Serikali inatambua gunia kuwa kipimo au kifungashio kwa mujibu wa sheria.

“Kwa mujibu wa sheria ya vipimo (The Weights and Measures Act Amendment)……
chini ya kifungu cha (2) (b) cha jedwali hilo ambacho kinasema mazao ya mashambani yatafungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu 100 pamoja na kuelekeza wauzaji na wanunuzi wa mazao kutumia mizani, Serikali haitambui gunia kuwa kipimo bali ni kifungashio,”

“Hivyo nitoe wito kwa wadau wote kuepuka matumizi ya gunia kama kipimo kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria va vipimo.” amesema Naibu Waziri Kigahe.

#Bunge