Mtanzania asajiliwa Shakhtar Donetsk inayoshiriki UEFA

0
476

Shakhtar Donetsk ya Ukraine imemsajili kwa mkopo kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas akitokea Zulte Waregem ya nchini Ubelgiji.

Novatus alitambulika kwenye soka la kulipwa akiwa Azam FC ambapo baadaye alisajiliwa Maccabi ya nchini Israel mwaka 2020.

Msimu wa 2021/22 alicheza kwa mkopo Beitar Tel Aviv ya Israel na majira ya joto mwaka 2022 alijiunga na Zulte kwa mkataba wa miaka mitatu.

Shakhtar Donetsk inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo imepangwa kundi moja pamoja na FB Barcelona, FC Porto na Royal Antwerp F.C.

Kinda huyo wa Kitanzania alizaliwa Septemba 2, 2002, na alichezea timu ya Taifa mchezo wake wa kwanza Septemba 2, 2021.