Mapigano Tripoli yaua watu 174

0
264

Watu 174 wamekufa na wengine 758 wamejeruhiwa wakati wa mapigano baina ya wapiganaji wanaomuunga mkono Mbabe wa kivita nchini Libya, – Jenerali Khalifa Haftar na vikosi vya serikali.


Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa Raia 14 ni miongoni mwa watu waliokufa katika mapigano hayo.


Mapigano hayo yalizuka Aprili Nne mwaka huu wakati Wapiganaji hao wanaomuunga mkono Jeneraki Haftar kutaka kuchukua udhibiti wa mji Mkuu wa Libya, – Tripoli.


Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa na kuendelea kwa mapigano hayo katika mji huo wa Tripoli na kutaka yasitishwe mara moja.