Uwanja wa Amaan kukamilika Desemba

0
398

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Amaan umefikia hatua nzuri ya kuridhisha na utakamilika kwa wakati (Disemba mwaka huu).

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo na kueleza kuwa matarajio ya Serikali ni kuwa sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari mwakani zitafanyika katika uwanja huo.

Baada ya ukarabati, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 15,500, na utakuwa na viwanja viwili vidogo vya mpira wa miguu.

Kwa upande mwingine, uwanja huo pia utatumika kwa michezo mbalimbali yenye hadhi ya kimataifa ikiwemo mpira wa miguu , netiboli, mpira wa wavu, mpira wa meza, pamoja na mchezo wa judo.