Tamasha la Kizimkazi kufunguliwa leo

0
328

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, Leo anatarajiwa kufungua Tamasha la Kizimkazi linalofanyika Paje wilaya ya Kusini mkoa Kusini Unguja.

Tamasha hilo linafanyika Paje ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati wa tamasha kama hilo mwaka 2022 ambapo alisema ni vema tamasha la Kizimkazi lifanyike katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Kusini ili kutoa fursa ya maendeleo.

Lengo la Tamasha la Kizimkazi ni kuunganisha Wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kabla ya ufunguzi rasmi wa tamasha lilo Rais Mwinyi ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa jengo la hospitali ya Kizimkazi, Mkunguni.

Kilele cha Tamasha hilo ni Agosti 31, 2023 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.