Mason Greenwood kuondoka Manchester United

0
313

Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na mshambuliaji Mason Greenwood, baada ya uchunguzi wa ndani wa miezi sita kuhusu tabia yake.

Greenwood alikamatwa Januari 2022 kwa tuhuma zilizohusiana na habari zilizochapishwa mitandaoni kuhusu jaribio la ubakaji na unyanyasaji.

Mashtaka dhidi ya mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 21 yalifutwa Februari 2023.

Licha ya kufutwa kwa mashtaka dhidi yake, klabu hiyo ilisema kuwa “wote waliohusika, ikiwa ni pamoja na Mason, wanatambua ugumu wa yeye kuanza tena kazi yake Manchester United.

“Hivyo, imeafikiwa kwa pande zote kwamba ingekuwa sahihi zaidi kwake kufanya hivyo mbali na Old Trafford, na sasa tutashirikiana na Mason kufikia matokeo hayo.”