Wengi wanasubiri Askofu Shoo atasema nini leo

0
170

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo amesema Kanisa hilo linaunga mkono uwekezaji na kuwa halipingi uwekezaji.

Dkt. Shoo amesema hayo mkoani Arusha alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na kuongeza kuwa kanisa hilo linafahamu nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ni uwekezaji.

Amesema katika suala la DP World kanisa linaunga mkono uwekezaji huo japo suala hilo limekuwa na maoni mbalimbali, na wao kama viongozi wa dini awali waliomba kuonana na Rais ili kutoa maoni yao katika suala hilo hivyo wanaamini maoni waliyotoa yatafanyiwa kazi kama ilivyokuwa ahadi ya Rais Samia kuwa yatafanyiwa kazi kwa uzito unaostahili.

“Sasa najua wapo tu watu wengi wanasubiri hivi Shoo atasema nini leo…..kwamba eti atasema nini KKKT atasema nini……
Lipo hili la DP Wolrd Mheshimiwa…. kwanza naomba tu ieleweke wazi kwamba kanisa linaunga mkono uwekezaji. Hatupingi uwekezaji Mheshimiwa Rais, na tunajua wewe kwenye nia yako unataka wawekezaji,”

“Hata hivyo jambo hili limekuwa na maoni mbalimbali ya Wananchi na vyombo vya habari, kwenye mitandao na kadhalika tumeona maoni mbalimbali. Lakini Mheshimiwa Rais unatambua sisi viongozi wa dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni kabisa mwa jambo hili.
……..na kwa uungwana wako, na kwa unyenyekevu ulionao, utayari wa kusikiliza ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama taasisi na viongozi wakuu wa dini katika nchi yetu ya Tanzania madhehebu yote ya kikristo tukiwa CCT, tukiwa TEC, tukiwa BAKWATA”.
Amefafanua Dkt. Shoo na kuongeza kuwa

“Mimi nakumbuka jinsi ulivyotupokea ukatusikiliza, ukapokea maoni yetu na ushauri wetu viongozi wa dini na ukaahidi kuwa maoni na ushauri huo utapeleka kwa wataalamu na kufanyiwa kazi kwa uzito unaostahili kwa maslahi mapana ya Taifa”.