Mradi wa Afya Kamilifu wazinduliwa Tanga

0
288

Shirika la Utafiti wa Tiba na Afya Barani Afrika (AMREF) lina mpango wa kushirikiana na viongozi wa dini katika maeneo wanayotoa huduma, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kutoa huduma endelevu za Ukimwi na Virusi vinavyosababisha Ukimwi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Dkt Florence Temu wakati wa uzinduzi wa mradi wa Afya Kamilifu.

Dkt Temu amesema kuwa katika kipindi cha miezi Sita iliyopita kwa mkoa wa Tanga pekee, AMREF imeweza kuwafikia watu 3, 129 wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Ukimwi na ambao hawatumii dawa za kufubaza virusi hivyo.

Mkoa wa Tanga umekua na ongezeko la watu wanaoishi na Virusi vinavyosababisha Ukimwi, ambapo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita maambukizi hayo yamepanda kutoka asilimia 2.4 hadi kufikia asilimia Tano.