Matatizo ya meno yahusishwa na afya ya akili

0
213

Utafiti mpya kutoka chuo Kikuu cha Tohoku cha nchini Japan umebainisha kuwa matatizo ya meno yanaweza kusababisha kusinyaa kwa sehemu ya ubongo inayodhibiti kumbukumbu na uwezo wa kujifunza.

Hii ina maana kuwa pasipokuwa na matunzo mazuri ya fizi na meno inaweza kusababisha tatizo la akili na hata wakati mwingine kuugua ugonjwa ufahamika kama Alzheimer [ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu] pale mtu anapofikisha umri wa makamo na uzee.

Utafiti huo uliochapishwa mwaka 2022 katika jarida la ‘Neurology’ umefanywa kwa takribani miaka minne ukihusisha washiriki 172 wenye umri wa wastani wa miaka 67.

Tafiti mbalimbali nazo zimehusika kuchunguza zaidi uhusiano kati ya afya ya meno na utendaji kazi wa ubongo, ambapo moja ya tafiti hizo iliyochapishwa mwaka 2021 imebainisha kuwa wazee wanapopoteza meno kutokana na uzee hatari ya kupata tatizo la utambuzi ambayo ni shida ya afya ya akili huongezeka pia huku mwingine wa mwaka 2022 ukibainisha kwa upande wa wanyama pale wanapopoteza jino husababisha kuzotota kwa mfumo wa neva.