CRDB yapata faida ya Shilingi Bilioni 64

0
567

Benki ya CRDB imepata faida ya Shilingi Bilioni 64 kwa mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 78 kutoka faida ya Shilingi Bilioni 36 iliyoipata mwaka 2017.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa mkutano wa kuwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2018 kwa wafanyakazi na waandishi wa habari.

Aidha Benki hiyo kupitia taasisi yake ya Microfinance inatarajia kuwawezesha wajasiriamali wengi zaidi, kwa kuwa imetenga takribani Shilingi Bilioni 400 kwa ajili ya wajasiriamali wa kati na wadogo ili kuwawezesha kukuza uchumi binafsi na wa Taifa.