Dkt. Mwinyi : Tutahakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya

0
595

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema malengo ya Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua kituo cha afya Bumbwini Makoba wilaya ya Kaskazini B mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Dkt. Mwinyi amesema katika hatua za awali zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora ili kufikia malengo ya kuimarisha miundombinu kwa kujenga hospitali za wilaya kila wilaya, hospitali za mkoa kila mkoa na hospitali ya Binguni itakayokuwa kubwa zaidi na kutoa huduma za uchunguzi Zanzibar.