Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas Ahmed kusimamia utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme katika wilaya ya Newala mkoani humo, unaotekelezwa na Mkandarasi Central Electric International Company ambaye alipaswa kukamilisha mradi huo mwezi Aprili mwaka huu.