MAMA MARIAM MWINYI AGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI

Zanzibar

0
196

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi
amesema taulo za kike za Tumaini Kits zinazotolewa na taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
zina lengo la kuwasaidia Wasichana wakati wa masomo yao waweze kufanya vizuri na kujistiri ikiwa ni pamoja na kuwa salama kwa afya ya uzazi na kutunza usafi wa mazingira.

Mama Mariam Mwinyi
ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi ya ZMBF
ameyasema hayo katika hafla ya ugawaji wa Taulo za kike za Tumaini katika shule ya Kijini wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema ZMBF leo imehitimisha kampeni iliyoianza siku ya Hedhi Salama Duniani iliyoadhimishwa Mei 28, 2023 kwa ugawaji wa vifurushi vya Tumaini 562 kwa wasichana wa shule za msingi na sekondari Kijini pamoja na shule ya sekondari Potoa.

Ametoa rai kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuiunga mkono programu ya Tumaini Initiative ambayo ina lengo la kuwafikia Wanafunzi elfu 20 kwa mwaka ambapo hadi sasa wamefikiwa 1,557 ndani ya kipindi cha miezi minne kwa ushirikiano na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Taasisi ya WAJAMAMA ambao ni wabobezi wa kutoa huduma na elimu ya afya ya uzazi.