Mwenge watoa salamu za heshima kaburi la JPM

0
159

Mwenge wa Uhuru leo unahitimisha mbio zake mkoani Geita kwa kupitia miradi saba wilayani Chato, miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 13.

Ukiwa katika wilaya hiyo ya Chato, Mwenge wa Uhuru umetembelea Kaburi la Rais wa Tano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na kutoa salamu za heshima.

Mkoani Geita, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa muda wa siku 6 na kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 59 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 29.

Mwenge huo wa Uhuru unatarajiwa kuanza kukimbizwa mkoani Kagera kesho Agosti 8,2023, ukitokea mkoani Geita.