Mtanzania ang’ara Marekani dhidi ya Miami ya Messi

0
355

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Dallas inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani, Bernard Kamungo ameendelea kuwa gumzo kutokana na uwezo wake ambapo usiku wa kuamkia leo aliifungia timu yake goli katika sare ya 4-4 dhidi ya Inter Miami anayochezea Lionel Messi.

Kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma alikocheza soka mtaani hadi kucheza soka nchini Marekani, safari yake inaonekana kama filamu ya michezo yenye mabonde na milima.

Kamungo alisajiliwa Dallas FC mwaka 2022 ambapo yeye na familia yake walihamia Texas, Marekani mwaka 2016.

Nyota huyo ameendelea kuwa na msimu mzuri ambapo Januari 2023 aliitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania.