Kuanzia sasa wananchi waingie nanenane bila kulipa

0
169

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametangaza rasmi wananchi kuingia katika viwanja vya maonesho na sherehe za Nanenane bila malipo.

Dkt. Mpango ametoa tangazo hilo alipokuwa akifungua rasmi sherehe na maonesho hayo mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.

Dkt. Mpango amesema lengo la kuwepo kwa fursa ya maonesho hayo ni wananchi au wakulima wa kawaida kuona mazao pamoja na kukutana na fursa zilizopo katika viwanja hivyo.

Amesema kutoza fedha za viingilio ni kuwazuia wakulima na wananchi kwa ujumla jambo ambalo ni kinyume na malengo ya kufanyika kwa maonesho hayo