FIFA yaiondolea adhabu Fountain Gate FC

0
295

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limeiondolea klabu ya Fountain Gate FC adhabu ya kusajili wachezaji. Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo inayoshiriki Championship kumlipa madai yake yote aliyekuwa kocha wao Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman.

Kocha huyo raia wa Misri aliishitaki klabu hiyo kwa kumvunjia mkataba kinyume na taratibu, lakini baada ya makubaliano ya pande zote mbili ,FIFA imefuta adhabu hiyo.

Aidha Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) nalo limeiondolea Fountain Gate Fc adhabu ya kufungiwa usajili.

Uamuzi huo ni habari njema kwa klabu ya Fountain Gate FC na mashabiki wake, ambao watafurahia kuona klabu yao ikiwa na uwezo wa kusajili wachezaji wapya na kuendelea kushindana katika Ligi ya Championship.