Mageuzi Katika Taasisi ni Lazima

0
235

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema mageuzi katika taasisi za Serikali hayakwepeki, hivyo taasisi hizo zifahamu kuwa mageuzi hayo ni ya lazima.

Mchechu ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa mwaka 2021/2022 na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka 10 wa shirika hilo utakaoanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Amesema taasisi nyingine za Serikali ziige kutoka TANESCO ambayo imekuwa ya kwanza kuthubutu kufanya mageuzi makubwa ambayo yameanza kuzaa matunda.

Amesisitiza kuwa moja ya msingi wa mageuzi hayo ndani ya taasisi ni taasisi kuwa wazi hasa katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji ili Wananchi wengi zaidi wajue kipi kinafanywa na taasisi husika.

Mchechu amesema lazima mageuzi ndani ya taasisi zote za Serikali yaanzie kwenye uongozi.