Wananchi laki tano waunganishiwa umeme 2021/2022

0
149

Jumla ya Wananchi 504,366 nchini wameunganishiwa nishati ya umeme kwa mwaka 2021/2022, ikiwa ni rekodi ambayo haijawahi kutokea.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa taarifa ya mwaka 2021/2022 ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Maharage Chande amesema rekodi hiyo haijawahi kutokea hapo awali na hiyo inatokana na utendaji kazi mzuri wa watumishi wa Shirika hilo.

Amesema Watumishi wa TANESCO wamekuwa wakifanya kazi kwa kujituma kuhakikisha Wananchi wananufaika na huduma ya umeme.