Kampeni Ya Mama Samia Itasaidia Wanawake na Watoto.

0
179

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Zainab Shaibu amesema, kampeni ya Mama Samia ya utoaji wa huduma za Msaada wa Kisheria zitawasaidia Wanawake na Watoto kwenye kesi za mirathi, ardhi na matukio ya unyanyasaji.

Zainab amesema hayo kwa niaba ya wajumbe wa UWT Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti Mary Chatanda walipokuwa wakikagua utekelezaji wa kampeni hiyo katika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akisoma taarifa ya utokelezaji wa kampeni hiyo Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Ester Msambazi amesema, zaidi ya Wananchi elfu 34 wamefikiwa katika kipindi cha siku nane mkoani Ruvuma huku Wananchi 516 wakipata msaada wa kisheria.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema kampeni hiyo ya Mama Samia ya utoaji wa huduma za Msaada wa Kisheria
imebaini migogoro ya aina nne inaongoza ambayo ni ya ardhi, mirathi, ndoa na ukatili wa kijinsia ambapo waathirika ni Wanawake na Watoto.