Mnara mrefu zaidi Afrika kujengwa uwanja wa Mashujaa

0
229

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan amesema amevutiwa zaidi na ramani ya uwanja wa Mashujaa, Dodoma ambapo jambo la kipekee na kubwa zaidi katika ramani hiyo ni ujenzi wa mnara mrefu zaidi Afrika katika uwanja huo uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambapo maadhimisho hayo yamefanyika pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mnara wa Mashujaa.

“Kabla sijaanza shughuli hii nilipofika nilioneshwa ramani ya uwanja huu utakavyokuwa. Nimevutiwa sana na ramani ya uwanja wa Mashujaa, uwanja huu utakuwa na migahawa ya kimataifa. Kutakuwa na kumbi za mikutano, kutakuwa na vivutio vingine vya watu kupumzika na kupata burudani kama michoro ilivyoonesha,” Amesema Rais Samia na kuongeza kuwa

“Kubwa zaidi utakuwa na Mnara mrefu kabisa ndani ya Afrika yetu labda ujengwe mwingine kabla wetu haujakamilika, lakini kama wetu utakamilika mwanzo…. utakuwa na sifa hizo za kuwa mnara mrefu kabisa ndani ya Afrika.“