Hifadhi ya Gesi, Ghuba ya Yamal, Urusi

0
519

Uwekezaji katika teknolojia na rasilimali watu ni nyenzo muhimu katika uzalishaji wa nishati safi ambayo inatajwa kuwa mkombozi katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabianchi.

Kampuni ya Gazprom ya nchini Urusi inayojihusisha na utafutaji, uziduaji na usambazaji gesi asilia imesema uwekezaji huo una tija hasa katika mnyororo mzima wa thamani wa gesi asilia.

Imesema kupitia utafiti walioufanya waligundua hifadhi ya gesi asilia yenye mita za ujazo Trilioni 20 katika eneo lote la Ghuba ya Yamal na bahari ya Kara.

Katika eneo jingine la Bovanenkovskoye
uendelezaji wa uwekezaji ulianza mwaka 2012 katika eneo lenye ukubwa wa kilomita 1,780.

Katika eneo hilo jumla ya visima 770 vilipangwa kujengwa na mpaka sasa tayari visima 700 vimeshajengwa.

Katika eneo hilo shughuli kuu zinazofanyika ni kuzidua gesi, kuchakata na kuiweka katika presha inayohitajika na kusafirisha mpaka katika kituo cha kupokea gesi ambako baada ya kufika katika kituo hicho cha kampuni ya Gazprom ndiko shughuli za usambazaji kitaifa na kimataifa hufanyika.

Takribani watu elfu moja wameajiriwa katika mradi wa Bovanenkovskoye pekee ambao ni mradi mmoja kati ya mitatu iliyopo katika Ghuba ya Yamal.