TANZANIA IPO MBELE MASUALA YA TEHAMA

0
142

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema Tanzania ipo mbele ikishughulikia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Dkt. Rioba ameyasema hayo wakati akiendesha kongamano la majadiliano ya ripoti ya Haki Jinai liliofanyika katika ukumbi mpya wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Wale tunaofahamu na tunaofuatilia Tanzania ipo mbele sana kwenye mambo ya TEHAMA, ukweli kwamba tunaye Waiziri hapa anayeshughulika na masuala ya TEHAMA ni ushahidi kwa namna ambavyo nchi yetu inathamini sana kubadilisha mifumo ya kwenda na teknolojia ya kisasa,” amesema Dkt. Rioba.