Mkuchika aomba meli Mtwara

0
166

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu-Kazi Maalum George Mkuchika amemuomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo @daniel_godfrey_chongolo kuweka mkazo kwenye suala la kuwezesha bandari ya Mtwara kuwa na meli itakayokuwa inafanya safari za ndani na Taifa jirani la Comoro ambalo limekuwa mshirika mkubwa wa kibaishara kupitia mkoa wa Mtwara.

Waziri Mkuchika amesema hayo mkoani Mtwara wakati anatoa salamu za Wananchi wa Mtwara, kwenye mkutano wa hadhara kwa Katibu Mkuu huyo wa CCM kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Amesema hamu ya Wananchi wa Mtwara ni kupata meli moja au mbili za uhakika ili kuendeleza uhusiano wa kibiashara na Taifa la Comoro.

“Ipatikane meli inayoenda Comoro, na mimi niko serikalini na nilifuatalia sana, walisema ziwa Victoria tumemwaga mameli, ziwa nyasa tumemwaga mameli, ziwa Tanganyika tumemwaga mameli, bahari ya hindi huku tupate meli hata moja au mbili ili tufanye biashara na ndugu zetu wa Comoro,” amesema waziri Mkuchika