“Mkisoma kwenye mitandao ya kijamii tunakosolewa kushoto kulia mpaka nje ya nchi, sasa wale mnaohisi wana mchango mzuri mnaweza mkawaleta wakawa sehemu ya mipango, wakafikiri pamoja na sisi ili kuondoa lile vuguvugu wanalosema wamepanga nini….
Leteni list yao tuwafanyie veting tuwaweke kwenye Tume ya Mipango”.
“Kuna msemo unasema maendeleo ni suala la haki ya binadamu na haiepukiki. Tunapotaka Tanzania ya maendeleo lazima tukae, tupange ili tufikiri. Niwaombe msiende kuona woga kufikiri wala kuja na mapendekezo ambayo mnaona yanaweza kuiendesha Tanzania vizuri”.
Wakati sisi tunalumbana bandari apewe nani.. iende isiende wenzetu kwa kuona malumbano yetu mmeona wameenda kulekule na lile jumba liliwekwa bendera ya Tanzania limewekwa ya jirani, sasa kama Tanzania tumeuza na wale jirani wameenda kufanya nini?. Na siku ambayo bunge letu hapa lilisema kuwa ni ruhusa bandari iendeshwe na private sector siku ya pili wenzetu wakasema nyinyi moja lakini sisi zote ziende huko na wakakimbia kule kwenda kuiwahi nafasi”.