Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Leo ameongoza hafla ya kuwaaga wapanda mlima 61 wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kampeni ya kuchangisha fedha za Mapambano dhidi Ukimwi katika geti la Machame wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) kwa kushirikiana na kampuni ya Geita Gold Mining ambapo inahusisha wapanda Mlima Kilimanjaro 36 na waendesha baiskeli 25.
Akiwaaga wapanda mlima hao Rais Mstaafu Kikwete amewataka Watanzania wanaotumia dawa za kufubaza virusi vinavyosababisha Ukimwi kuepuka kuchukua dawa katika maeneo yasiyo rasmi ili kuepuka kupata athari zaidi za ugonjwa huo.